Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bocco atwaa tuzo ya IDFA

Bocco Ashinda Tuzo John Bocco ashinda Tuzo ya IDFA

Mon, 22 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa Simba SC, John Bocco ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka 2020 wa Mashabiki zilizotolewa na Chama cha Soka Wilaya ya Ilala (IDFA).

Bocco amewashinda mlinda mlango Aishi Manula na mlinzi wa kushoto Mohamed Hussein Zimbwe Jr katika hafla ya tuzo hizo zilizofanyika Ukumbi wa Hoteli ya Ramada jijini Dar es Salaam.

Msimu wa mwaka 2020/21 ulikuwa bora kwa Nahodha Bocco kutokana na kushinda tuzo nyingi binafsi kama mfungaji bora wa ligi na mchezaji bora wa mwaka (MVP).

Katika hafla hiyo pia klabu ya Simba SC imeshinda tuzo ya klabu bora ya mwaka kutokana na mafanikio makubwa waliyoyapata.

Msimu wa 2020/21 Simba SC ilicnyakua mataji yote ya ndani Ligi Kuu, Azam Federation Cup, Ngao ya Jamii na kufika robo fainali ya michuno ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live