Francesco Totti alidumu AS Roma miaka 24, kila benchi la ufundi lililokuja lilimpa heshima yake, iwe kumpa nafasi ya kucheza ama lah, alikuwa kipenzi cha viongozi na mashabiki na nahodha wa mfano, hadi pale alipoufuata uongozi na kuomba kutundika daruga.
Pale Bayern Munich hadi leo Thomas Muller na umri wake wa miaka 34, no matter kuna nyakati anasugua benchi ama anapewa dakika 10 pekee za kucheza bado klabu inaamini yeye ni wa thamani sana, uwepo wake kwenye timu una maana kubwa.
Heshima aliyoipata Totti na anayoendelea kuipata Muler ni tofauti kabisa na ilivyo kwa John Bocco. Anapopolewa maneno makali kuanzia uwanjani hadi mitandaoni.
Guys inawezekana Bocco hana hiyo energy, hana huo ubora, lakini nani anajua uzito wa kauli yake kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwa wenzake?
Nani anajua ushawishi wake kwa wenzake? Nani anajua nguvu zake za kuwapambania wenzake kupata haki sawa? Nani anajua ilivyo bond yake kati yake na uongozi kuja kwa wachezaji hadi kwenye benchi la ufundi?
Tumejiuliza kwa nini kila kocha ameendelea kumuachia kitambaa kama nahodha mkuu? Football sio dakika 90 pekee kwenye pitch.
Legends huwaondolewi kiholela kama fungu la nyanya kwa pamoja. Ni miezi kadhaa tu kaondolewa Jonas Mkude. Ishu sio fadhila, bali umuhimu wake ambao sio rahisi kila mtu kuuona.