Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bocco anastahili heshima yake

Bocco Bao 3 Bocco anastahili heshima yake

Wed, 27 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

John Rafel Bocco Mfungaji bora wa muda wote wa Ligi Kuu Tanzania akiwa na magoli 154, akifunga kwenye misimu 16 mfululizo tangu alipoanza kucheza Ligi Kuu akiwa na AZAM FC mwaka 2008/09 baada ya kuipandisha Daraja Azam FC.

John Bocco alivunja rekodi ya Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ aliyekua anashikilia rekodi hii kwa kua na magoli 153 katika misimu 13 mfululizo.

Mmachinga aliweka rekodi yake kati ya mwaka 1993-2005 alipostaafu baada ya kuchezea klabu za Bandari Mtwara, Yanga SC, Simba SC, Mmbanga FC na Twiga Sports.

John Rafel Bocco amecheza Simba SC tangu mwaka 2017 na ameifungia Simba SC magoli 70.

John Bocco ana stahili Crown ya Ligi Kuu kama Mfungaji Bora wa muda wote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live