Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bocco aanika kilichowaua, Makwaya aikosoa beki Simba

94921 Pic+simbazz.png Bocco aanika kilichowaua, Makwaya aikosoa beki Simba

Mon, 10 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

BAADA ya kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania, Nahodha wa Simba, John Bocco amesema walijichanganya na kuruhusu bao hilo huku nahodha wa JKT, Damas Mwakwaya akifunguka udhaifu walioonyesha Simba katika mchezo huo. Simba inaongoza Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 50 imekubali kipigo hicho katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Uhuru ambapo wapinzani wao walifunga bao hilo pekee dakika ya 24 kipindi cha kwanza kupitia Adam Adam. Adam aliunganisha mpira wa krosi iliyochongwa na mchezaji mwenzake na kujaa wavuni licha ya kipa, Beno Kakolanya kujaribu kuchumpa kuucheza. Baada ya bo hilo, Simba ilipambana kusaka bao la kusawazisha na kukutana na kigingi kutoka kwenye ngome ya ulinzi ya JKT Tanzania. Baada ya ya mchezo huo, Bocco aliwapongeza wapinzani wao kwa ushindi huo akibainisha kwamba walijichanganya na kuruhusu bao. "Baada ya kufungwa tulijaribu kupambana kupata matokeo lakini imelindikana, JKT walijipanga vizuri na wanastahili pongezi," alisema Bocco na kuongeza kwamba wanajipanga kwa ajili ya mechi zijazo. Nahodha na beki wa JKT Tanzania, Damas Makwaya alisema mpango walioingia nao umefanyakazi kwani wamepata matokeo mazuri waliyoyatarajia ambapo kabla ya kuingia uwanjani kocha wao Mohamed Abdallah 'Bares' aliwaelekeza jinsi ya kuwabana wapinzani wao. "Alituelekeza tuwabane sana Simba, mpira ulivyoanza walikuwa kawaida, tukaona tuna uwezo wa kuwamudu na beki yao ilikuwa dhaifu," alisema na kuendelea. "Washambuliaji wetu walikuwa na kasi, hivyo tukatumia faida hiyo kusaka bao tumefanikiwa na kupata pointi tatu," alisema .

Chanzo: mwananchi.co.tz