Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bocco, Phiri watembeza 'boli' Ushirika Moshi

BBEF590E 3EF3 4167 B863 F2D2EEB6BF7D.jpeg Moses Phiri amefunga mabao mawili mchezo wa leo

Sun, 27 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Polisi Tanzania kimeanza vibaya katika Uwanja wa Ushirika uliokuwa umefungiwa kupisha marekebisho baada ya kukubali kichapo cha magoli 3-1 kutoka kwa Simba SC.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC ulishuhudia dakika za mwanzo za mchezo kila timu ikianza kwa kasi huku wakishambuliana kwa zamu.

Alikua ni John Bocco aliewatanguliza Simba kipindi cha kwanza akimaliza pasi safi ya Shomari kapombe kabla ya Phiri kuongeza bao la pili akitengenezewa na Clatous Chama.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika Simba walikua mbele kwa uongozi wa mabao 2-0.

Kipindi cha Pili Simba walirudi kwa kasi na kupata bao la tatu kupitia kwa Mzambia Moses Phiri na kuwanyong'onyeza wenyeji.

Dakika ya 90 Polisi Tanzania walipata bao la kufutia machozi na mpaka dakika 90 zinakamilika Simba wakafanikiwa kuondoka na alama tatu na kuwafanya wafikisha pointi 31 katika msimamo wa Ligi na kusogea mpaka nafasi ya pili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live