Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bocco, Mugalu kuiongoza Simba dhidi ya Kaizer

Kikosi Pic Data Bocco, Mugalu kuiongoza Simba dhidi ya Kaizer

Sat, 22 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

NAHODHA wa klabu ya Simba John Bocco 'Adebayo' ni miongoni mwa wachezaji wa kikosi hicho wanaoanza katika mchezo wa leo Mei 22, 2021 dhidi ya Kaizer Chiefs.

Saa 10:00 jioni Simba anashuka katika dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam kuwakabili Kaizer Chiefs mchezo wa pili wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba inahitaji kupata matokeo katika mchezo wa leo zaidi ya bao 5-0 ili waweze kumuondoka Kaizer Chiefs aliyeshinda 4-0 katika mchezo wa kwanza.

Mbali na Bocco, nyota wengine wanaoanza katika kikosi hicho ni Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Joash Onyango, Paschal Wawa, Thadeo Lwanga, Clatous Chama.

Wengine ni Mzamiru Yassin, Chris Mugalu na Luis Miquissone huku nyota wa akiba Beno Kakolanya, Erasto Nyoni, Kennedy Juma, Said Ndemla, Bernard Morrison, Miraji Athuman, Meddie Kagere, Larry Bwalya na Francis Kahata.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz