Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bocco, Erasto watemwa Taifa Stars

John Bocco Simbascnews Bocco, Erasto watemwa Taifa Stars

Tue, 15 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KOCHA wa timu ya Taifa Tanzania, Kim Poulsen amewaacha wachezaji wakongwe John Bocco na Erasto Nyoni katika kikosi chake kinachoingia kambini Jumapili kwa ajili ya mechi za kufuzu Chan na AFCON.

Kim amesema amewaacha nyota hao lakini bado wana nafasi ya kumshawishi kwenye mechi zao zijazo ili aweze kuwarejesha kikosini.

Kocha huyo amesema licha ya kukosekana kwa wachezaji hao amewajumuisha wachezaji wengine ambao anaamini watafanya vizuri.

“Erasto na Bocco hawatokuwepo lakini bado wana nafasi ya kurejea wakati tukiwa kambini na bado kuna muda kabla ya kucheza mashindano yetu,” amesema Kim

Kim amesema kikosi chake kitacheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Afrika ya Kati na Sudan inayotarajiwa kuchezwa Machi 23 na 29.

Wachezaji walioitwa ni Aishi Manula, Metacha Mnata, Abuutwalib Mshery, Shomari Kapombe, Israel Mwenda, Haji Mnonga, Dickson Job, Mwamnyeto, Lusajo Mwaikenda, Abdulrazack Mohamed, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Nickson Kibabage na Farid Mussa.

Viungo ni Novatus Dismas,Mzamiru Yassin, Jonas Mkude, Andabwile Aziz, Zawadi Mauya na Feisal Salum.

Mawinga ni Mbwana Samatta, Simon Msuva, Ben Starkie na Kelvin John. Upande wa ushambuliaji George Mpole, Reliants Lusajo, Ibrahim Joshua na Kibu Denis.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live