Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Boca Juniors mabingwa Ligi Kuu ya Argentina

Boca Juniors Boca Juniors mabingwa Ligi Kuu ya Argentina

Tue, 25 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Boca Juniors imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Argentina baada ya kupata sare ya kufungana bao 2-2 na Independiente na kufikisha alama 52 huku wapinzani wao Racing Club walipoteza kwa kufungwa na klabu ya River Plates mabao 2-1 na kusalia na alama zao 50 katika nafasi ya pili.

Utakumbuka msimu uliopita Boca Juniors walifanya vibaya sana na kumaliza Ligi wakiwa katika nafasi ya 4 huku klabu ya River Plates wakitwaa ubingwa ambapo msimu huu wa 2022 wamemliza nafasi ya tatu.

Ligi hiyo ya Argentina itamalizika rasmi Oktoba 26 kwa michezo mwili kupigwa mmoja ukiwa wa kiporo kati ya Velez Sersfield dhidi ya Central Corboba na mchezo wa mwisho wa kukamilisha ratiba utakuwa kati ya Platense dhidi ya vibonde Lanus.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live