Kocha wa zamani wa timu ya Taifa Ufaransa, Laurent Blanc amefutwa kazi kama kocha mkuu wa klabu ya Olympique Lyon kufuatia mwenendo usioridhisha wa klabu hiyo kwenye Ligi Kuu Ufaransa.
Blanc ambaye aliteuliwa kuiongoza klabu hiyo mnamo Oktoba 2022 na kuiongoza Lyon kumaliza nafasi ya tatu msimu uliopita alianza msimu huu vibaya akipoteza mechi tatu na sare moja kwenye mechi nne za ufunguzi wa Ligue 1.
Lyon itakuwa chini ya msaidizi wa Blanc, Jean-Francois Vulliez, huku mmiliki mpya wa klabu hiyo, Mmarekani John Textor akiendelea kumsaka mrithi wa Blanc.
Kiungo wa zamani wa Italia Gennaro Gattuso, ambaye amekuwa hana kazi tangu alipoondoka Valencia mwanzoni mwa mwaka huu na mkufunzi Oliver Glasner aliyeondoka Eintracht Frankfurt mwishoni mwa msimu uliopita, wote wanahusishwa na kibarua hicho.