Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bizimungu: Simba wametuharibia bajeti

40236 Pic+mechi Bizimungu: Simba wametuharibia bajeti

Tue, 5 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

 KOCHA mkuu wa Mwadui, Ally Bizimungu amesema kubadilishwa kwa ratiba ya mchezo wao dhidi ya Simba, kumewavurugia bajeti waliyokuwa wameiandaa ya kukaa mjini hapa.

Simba na Mwadui zilitakiwa kucheza Jumatano lakini mchezo huo umesogezwa mbele na kuchezwa Alhamisi baada ya msafara wa wachezaji wa Simba kuingia kwa mafungu wakitokea nchini Misri. "Tulipanga bajeti ya siku tano mpaka sita lakini kusogezwa kwa mechi yetu kunatufanya bajeti iongezeke na kuwa siku saba, hii haipo sawa kabisa wametuvuruga kiuchumi," alisema.

 Akizungumzia mchezo wenyewe alisema kwamba anatambua ugumu uliopo kutokana na Simba wanahitaji kuwatuliza mashabiki wao.

"Simba wametoka kupoteza huko kwahiyo hapa watataka kupata matokeo mazuri ili kuwatuliza mashabiki wao, lakini na sisi tutapambana ili kuhakiikisha tunatoka na ushindi au pointi yoyote,"alisema.



Chanzo: mwananchi.co.tz