Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Birthday ya Yanga kufanyika Mbeya

Yanga Supu974837 Birthday ya Yanga kufanyika Mbeya

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imepanga kufanya sherehe ya kuadhimisha miaka 89 tangu kuzaliwa kwake Februari 11, 2024, jijini Mbeya siku ambayo itakutana na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 5, 2024 jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ally Kamwe amesema tayari matukio mbalimbali kuelekea kilele cha maadhimisho hayo yameanza na kesho wanatarajia kuingia mkataba na hospitali kubwa nchini.

Amesema lengo la kuingia mkataba na hospitali hiyo ambayo hakuitaja jina ni kuweza kuwasaidia mashabiki wao katika suala la afya.

“Kesho Yanga inakwenda kusaini mkataba na hospitali kubwa sana duniani, ikiwa na lengo la kumnufaisha shabiki wetu kwenye masuala yanayohusu afya yao. Pia Jumatano tunazindua upya ofisi yetu pale Jangwani.

“Mkoa wa Mbeya umepata bahati ya kusheherekea ‘anniversary’ ya mabingwa wa kihistoria. Naomba mashabiki wote wa Yanga popote walipo wakaweke kambi Mbeya na tutazindua na nyimbo mbili kutoka kwa wasanii wakubwa,” amesema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live