Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bingwa EPL 2024/25 ni huyu

What Happens With The Premier League Trophy On The Final Day Of The Season Bingwa EPL 2024/25 ni huyu

Fri, 19 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Utabiri wa kompyuta juu ya timu gani itachukua ubingwa wa Ligi Kuu England msimu ujao unaonyesha kwamba matajiri kutoka Jiji la Manchester, Manchester City wataendeleza dozi na kuchukua taji lao la tano mfululizo la ligi hiyo.

Licha ya msimu huu kuwa na mabadiliko mengi kwa timu mbalimbali ikiwemo Liverpool na Chelsea ambazo zinaingia msimu ujao na mabenchi mapya ya ufundi baada ya kuwaajiri Arne Slot na Enzo Maresca.

Kompyuta hiyo ya Grosvenor Sport imetabiri kuna asilimia kubwa, Man City ikawa bingwa tena.

Kompyuta hiyo inatabiri msimamo wa mwisho kwa kuchezesha timu husika mchezo mmoja wa Ligi Kuu mara 1000, pia inazingatia kikosi cha timu na usajili inaofanya.

Kupitia vipengele hivyo, Manchester City imepewa asilimia 90 ya ubingwa ingawa utabiri huo unaweza kubadilika kadri timu pinzani zinavyosajili.

Arsenal iliendelea kutabiriwa kumaliza katika nafasi ya pili kama ilivyokuwa msimu uliopita ambapo walimaliza msimu na pointi 91, tatu pungufu ya mabingwa Man City waliomaliza na pointi 94.

Liverpool itakamilisha Top 3, wakati Erik ten Hag na vijana wake kutoka Old Trafford watamaliza katika nafasi ya nne, kwa mujibu wa utabiri huo wa kompyuta.

Kwa upande wa timu zinazoweza kushuka daraja, kompyuta imetabiri Ipswich Town itamaliza katika nafasi ya mwisho licha ya kufanya vizuri msimu uliopita ikiwa katika Ligi Daraja la Kkwanza ambako ilimaliza katika nafasi ya pili na kufanikisha mpango wa kumbakisha kocha wake Kieran McKenna aliyekuwa anawindwa na Chelsea kwa mujibu wa ripoti.

Mbali ya Ipswich, Wolves inatabiriwa kumaliza katika nafasi ya 19 ikiwa na pointi 29 ambazo ni 11 zaidi ya Ipswich, huku Nottingham Forest ikitabiriwa kumaliza katika nafasi ya 18.

Forest imetabiriwa kumaliza ligi na pointi 32 ambazo zitakuwa ni mbili pungufu ya Leicester City huku ikipishana pointi moja na Southampton na Brighton.

Chanzo: Mwanaspoti