Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Binadamu mwenye makombe mengi zaidi Duniani

Lionell Messi Binadamu mwenye makombe mengi zaidi Duniani

Tue, 16 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Lionel Messi ameendelea kuongeza kabati lake la makombe baada ya asubuhi ya jana kutwaa taji la Copa America 2024 na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye mataji mengi zaidi katika historia ya mpira wa miguu akifikisha jumla la makombe 45 na kuendelea kumwacha mbali beki wa zamani wa Barcelona na Brazil, Dani Alves kwenye makombe 43.

Licha ya kumaliza mechi ya fainali ya Copa America akiwa benchi kufuatia baada ya kupata majeraha, Messi ametwaa taji lake nne mfululizo kwenye michuano mikubwa ya kimataifa ambayo ni Copa America 2021, Finalisima 2022, Kombe la Dunia 2022 na Copa America 2024.

Messi alilaximika kutolewa mnamo dakika ya 66 ya mchezo wakati ubao ukisoma 0-0 kati ya Argentina dhidi ya Colombia kwenye mchezo huo wa fainali uliopigwa katika dimba la Hard Rock, Miami Marekani. Mchezo huo ulilazimika kuamuliwa kwenye dakika 30 za ziada baada ya dakika 90 kumalizika bila goli.

Bao la mshindi wa kiatu cha mfungaji bora wa michuano hiyo, Lautaro Martinez mnamo dakika ya 112 lilitosha kuipatia Argentina kombe la Copa America kwa mara ya 16 kihistoria na kuipita Uruguay yenye makombe 15.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live