Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bimenyimana na takwimu za kutisha Ligi Kuu Afrika Kusini

Bonfils Caleb Bimenyiman Mshambuliaji wa Kaizer Chiefs Bonfils-Caleb Bimenyimana

Mon, 16 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Kaizer Chiefs Bonfils-Caleb Bimenyimana ndiye mchezaji aliyecheza dakika chache zaidi, kati ya wachezaji watatu pekee waliofunga mabao zaidi ya matano kwenye Dstv Premiership msimu huu.

Caleb Bimenyimana (mabao 7 - dakika 613)

Peter Shalulile (mabao 7 - dakika 844)

Bredley Grobler (mabao 7 - dakika 1178)

Takwimu za Bimenyimana katika Dstv Premiership msimU huu;

michezo 9

dakika alizocheza 613

mabao 7

penati 4

pasi ya bao 1

ana wastani wa kufunga bao kila baada ya dakika 87

Bimenyimana ndiye mchezaji pekee aliyefunga hat trick kwenye Dstv premiership msimu huu hadi sasa, alifunga dhidi ya Stellenbosch October mwaka jana.

Kaizer Chiefs wamepata ushindi katika michezo yote minne ya Dstv Premiership ambayo Bimenyima alifunga bao msimu huu.

Bonfils-Caleb Bimenyimana ambae raia Burundi alijiunga na Kaizer Chiefs msimu akitokea FK Pohronie, ana miaka 25 na miongoni mwa nyota wanaofanya vyema katika ligi kuu nchini Afrika Kusini

Chanzo: www.tanzaniaweb.live