Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bilionea anayeitaka Chelsea ni huyu

Muhsin Bayrak.jpeg Bilionea anayeitaka Chelsea ni huyu

Mon, 7 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MFANYABIASHARA na bilionea kutoka Uturuki, Muhsin Bayrak, amepokea ofa ya kutaka kuinunua Klabu ya Chelsea na muda wowote atatua London kukamilisha mchakato huo.

Hii ikiwa ni siku chache baada ya tajiri wa Urusi na mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abramovich kutangaza kuiweka sokoni Chelsea. Chelsea imewekwa sokoni na dau lake likitajwa kuwa ni pauni bilioni 2.1. Abramovich akiwa na klabu hiyo tangu 2003, amefanikiwa kutwaa mataji 15.

Huyu anakuwa tajiri wa pili kutaka kuinunua klabu hiyo baada ya awali bilionea wa Uswisi, Hansjorg Wyss & LA Dodgers co-owner Todd Boehly kujitokeza kutaka kuinunua Chelsea.

Bayrak ambaye ni bilionea wa Kampuni ya Ujenzi ya AB Grup Holding, amethibitisha kuwa mpango wake wa kutaka kuinunua klabu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live