Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bilionea Qatar alisajilia kampuni Man United

Man United Mas Bilionea Qatar alisajilia kampuni Man United

Thu, 16 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bilionea kutoka Qatar, Sheikh Jassim bin Hamad al-Thani amesajili kampuni kubwa ya kifedha itakayokuwa chini ya Bank of America imsaidie kuamua ofa ya mwisho aliyotoa kuinunua Manchester United.

Vita ya kuinunua Manchester United imefikia katika hatua ya mwisho na taarifa zinadai kwamba mwekezaji huyo kutoka Qatar atatinga Old Trafford wiki hii kabla ya mpinzani wake Sir Jim Ratcliffe ambaye pia yupo katika mchakato wa kuinunua timu hiyo akichagizwa na uzawa kwa kuwa ni Mwingereza.

Sheikh Jassim amefanya uamuzi wa kujumuisha wawakilishi wake ambao ni benki hiyo watakapokutana na wamiliki wa sasa ambao ni familia ya Glazer kwa ajili ya mazungumzo ya kufanya biashara.

Kikao hicho kinatarajiwa kufanyika ndani ya saa 48 zijazo kabla ya kampuni ya Ineos inayomilikiwa na Ratcliffe kupeleka mawakala wake Old Trafford kesho kwa ajili ya uchunguzi wa kwanza wa taarifa mbalimbali za kifedha za klabu hiyo.

Mikutano ya mazungumzo kuhusu mchakato wa kuipiga bei Man United ilianzishwa siku 10 zilizopita wakati wawekezaji hao wawili walipoidhinishwa na kampuni ya Raine inayomilikiwa na familia ya Glazer. Wawekezaji Sheikh Jassim na Sir Ratclife, tajiri namba moja wa Uingereza waliweka mezani ofa ya kitita cha Pauni 4.5 bilioni kila mmoja.

Hata hivyo ofa hiyo inaaminika kuwa ni ndogo kwa sababu familia ya Glazer inataka kitita cha Pauni 6 bilioni ili iweze kuiachia klabu hiyo yenye histori tamu nchini humo.

Wiki iliyopita wafadhili wa kampuni ya Elliott Management walikuwa tayari kumfadhili mwekezaji yeyote ambaye atapenda kuinunua ili wasimamie mpango mzima wa mazungumzo.

Kampuni nyingine kama Ares Management, Oaktree na ‘MSD Parters zilikuwa tayari kujihusisha na biashara hiyo endapo wawekezaji hao wangekubali kuzihusisha.

Gazeti la Sun Sport lilifichua wiki iliyopita kuwa chaguo moja ambalo Glazers wanalizingatia ni kuiondoa sokoni Man United, badala yake wanataka kutumia mtaji wa nje kuanzisha kampuni mpya ili kuzuia uuzaji na uendeshaji wa biashara ya kidijitali.

Mpango huo wa familia ya Glazer utawaruhusu kupata pesa kutokana na fursa zinazowezekana kutoka kwa mauzo ya kidijitali, michezo ya video na leseni ya bidhaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: