Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bilbao kuikazia Barcelona kwa Nico

Nico Williams Barca Nico Williams

Thu, 18 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Vigogo wa Athletic Bilbao wameripotiwa kutaka kuhakikisha kwamba wanamzuia kiungo wao Nico Williams ambaye anawindwa sana na Barcelona katika dirisha hili.

Barca ina matumaini makubwa ya kumpata Nico na inadaiwa kuwa tayari kutoa hadi Pauni 53 milioni inayohitajika ili kuvunja mkataba wake.

Timu nyingi zimevutiwa na kiwango bora alichoonyesha staa huyu katika michuano ya Euro na licha ya kuwepo kipengele kinachomruhusu kuondoka hadi sasa bado hajafanya uamuzi wowote.

Barcelona imeripotiwa kumtumia hadi staa wao Lamine Yamal kumshawishi Nico kwa sababu wawili hao ni marafiki lakini hakuna kilichofikiwa muafaka hadi sasa.

Nico ambaye alicheza mechi 37 za michuano yote na kufunga mabao nane akiwa na Bilbao kwa msimu uliopita, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.

Wakati huo huo, Bayern Munich pia imeingia katika mazungumzo na wawakilishi wa kiungo wa RB Leipzig na Hispania, Dani OImo ili kumsajili katika dirisha hili.

Staa huyu ambaye Manchester City inamhitaji sana ili akawe mbadala wa Kevin de Bruyne anayeripotiwa kuwa hana muda mrefu wa kusalia kikosini hapo, alionyesha kiwango bora katika michuano ya Euro akiwa na Hispania hadi kufanikiwa kuchukua taji.

KIUNGO wa Real Sociedad na Hispania Mikel Merino ni mmoja kati ya wachezaji ambao Barcelona imepanga kuwasajili katika dirisha hili kiamini itampata kwa bei chee kwa sababu mkataba wake umebakisha mwaka mmoja kabla ya kumalizika.

Barca inaamini Sociedad italazimika kumuuza staa huyu kwa sababu kadri anavyozidi kukaa ndio anashuka bei na ifikapo mwisho wa msimu ujao anaweza kuondoka bure kabisa.

Hata hivyo, staa huyu pia anawindwa na Arsenal na Newcastle United.

NEWCASTLE United imepanga kuingia katika vita dhidi ya Everton kwa ajili ya kuipata saini ya winga wa Leeds United na Italia, Wilfried Gnonto, 20, katika dirisha hili baada ya kuridhishwa na kiwango bora alichoonyesha msimu uliopita. Gnonto ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Msimu uliopita alicheza mechi 44 za michuano yote.

Southampton imefikia makubaliano na West Ham kwa ajili ya kumsajili kiungo wa timu hiyo Flynn Downes, 25, katika dirisha hili ambapo itawagharimu kiasi kisichopungua Pauni 18 miliono kufanikisha mchakao wa kumpata.

Downes ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Msimu uliopita alicheza mechi 37 za michuano yote na kufunga mabao mawili.

BAYERN Munich haina mpango wa kumuuza winga wao Mathys Tel katika dirisha hili la majira ya kiangazi licha ya timu kibao za Ligi Kuu England kuonyesha nia ya kumsajili.

Inaelezwa kocha mpya Vincent Kompany amewaambia mabosi wa juu wa timu hiyo kwamba Tel ni mmoja kati wachezaji muhimu katika mipango yake kuelekea msimu ujao.

WEST Ham imewaweka katika rada zao washambuliaji watatu katika dirisha hili wakwanza ni kutoka Aston Villa, Jhon Duran, mshambuliaji wa Everton Dominic Calvert-Lewin na staa wa Arsenal, Reiss Nelson kwa ahiku ta kuboresha eneo lao la ushambuliaji.

Kwa mujibu wa ripoti kocha mpya Julien Lopetegui moja kati ya maeneo ambayo ameyabainisha kwamba yana mapungufu,

MABOSI wa West Ham wapo katika mazungumzo na Southampton kwa ajili ya kuipata saini ya beki wa timu hiyo, Kyle Walker-Peters katika dirisha hili.

West Ham ipo katika mchakato wa kutafuta beki wa kulia na chaguo lao la kwanza ni Walker-Peters ambaye wanaamini kamba watampata kwa bei chee na ikishindikana itahamia kwa beki wa Manchester United Manchester United, Aaron Wan-Bissaka.

STRAIKA wa Bournemouth, Kieffer Moore yupo katika nzuri kujiunga na Sheffield United baada ya kubadilisha uamuzi wa kutua Hull City katika dakika za mwisho.

Fundi huyu wa kimataifa wa Wales, mwenye umri wa miaka 31, mkataba wake unamalizika mwaka 2025. Bournemouth imekubali kulipa Pauni 8 milioni kwa ajili yake.

CRYSTAL Palace inataka kutuma ofa kwenda Sporting Lisbon, kwa ajili ya kumsajili winga wa timu hiyo Marcus Edwards kwa ajili ya kuziba pengo la Michael Olise ambaye amejiunga na Bayern Munich katika dirisha hili kwa Pauni 50.8 milioni.

Inaelezwa Palace imevutiwa na Edwards kutokana na kiwango bora alichoonyesha msimu uliopita ambapo alicheza mechi 44 za michuano yote na kufunga mabao sita.

@@@@@@@@

Uongozi wa Simba SC umefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na mshambuliaji Pa Omar Jobe, baada ya kipindi kifupi cha miezi sita.

Jobe (25) raia wa Gambia alisajiliwa Simba SC katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari akiwa mchezaji huru, baada ya kumaliza mkataba wake na timu ya Zhenis inayoshiriki Ligi Kuu nchini Kazakhstan.

Jobe ambaye alitarajiwa kufanya makubwa wakati akisajiliwa klabuni hapo, lakini alishindwa kuendana na kasi ya timu na malengo ya Simba SC, ambayo ilimaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara 2023/24.

Hata hivyo taarifa ya Simba SC imeeleza kuwa, katika kipindi chote alichokuwa na klabu hiyo alikuwa mchezaji msikivu, mwenye nidhamu ya hali ya juu na alikuwa anajituma mazoezini na uwanjani.

“Kuelekea msimu mpya wa mashindano 2024/25 tumefanya marekebisho makubwa ya kikosi na malengo yetu ni kurejesha makali tuliyokuwa nayo miaka minne iliyopita.

Simba inamtakia kheri Jobe katika maisha mapya ya soka nje ya Simba na siku zote tutaendelea kuthamini mchango wake ndani ya kikosi chetu.” Imeeleza taarifa ya Simba SC

Chanzo: Mwanaspoti