Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bila woga, Che Malone awataja viongozi wa Simba chanzo cha timu kuboronga

Che Malone Mangunguuu Che Malone na Mangungu.

Wed, 29 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa Kimataifa wa Simba SC raia wa Cameroon, Che Fondoh Malone Jr amesema kuwa sababu ya kikosi chao kufanya vibaya msimu huu ilikuwa ni maandalizi mabaya mwanzoni mwa msimu jambo ambalo lilisababisha kuanza msimu vibaya na kumaliza nafasi ya tatu kisha kuangukia michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Che Fondoh amesema hayo jana baada ya kutamatika kwa mchezo baina ya Simba dhidi ya JKT Tanzania, huku akiongeza kuwa sababu zilizopelekea timu hiyo kufanya vibaya msimu huu, ni uongozi pamoja na usajili wa wachezaji wa kiwango cha chini hivyo Simba wanapaswa kusajili wachezaji bora msimu huu kama wanataka kufanya vizuri kwenye mashindano watakayoshiriki.

“Siwezi kujua ni wapi tatizo limetokea lakini haikuwa vizuri na imetudhuru timu nzima hivyo ndivyo mpira ulivyo kila kitu ni kujiandaa na jinsi unavyo endesha klabu, naamini kulikuwa na maandalizi mabaya mwanzoni mwa msimu huu yaliyopelekea kuishia hapa tuliposhia.

“Kuhusu Simba kurudi vizuri msimu ujao itategemea na Menejimenti, itategemea na Pre Season itakavyokuwa, kwasababu jinsi utakavyojiandaa, Pre Season ndio itaamua msimu wako, itategemea na Menejimenti jinsi watakavyosajili wachezaji. Kadri unavyosajili wachezaji wazuri ndiyo unatengeneza mazingira mazuri ya kufanya vizuri, ninaamini msimu ujao utakuwa mzuri kwetu kuliko msimu huu.

“Kila beki niliyepangwa naye kucheza tulicheza vizuri, jambo kubwa ni mawasiliano na maelewano uwanjani. Ukiwa kama mchezaji lazima ujiandae kucheza na mtu yeyote ukayapewa naye kucheza kwa wakati wowote.

“Changamoto prkrr niliyoipata ni mawasiliano, kwa sababu sijui lugha vizuri (Kiswahili) lakini ninaamini kadri siku zinavyokwenda nitajitahidi kujiboresha na kuelewa lugha vizuri. Kwa sasa ninafahamu maneno machache kama mambo poa, tu;lia, twende, cheza hayo ni baadhi ya maneno ambayo nimeweza kuyashika haraka lakini nitaendelea kujifunza zaidi,” Che Malone.

Itakumbukwa kuwa mwanzoni mwa msimu uliomalizika, Simba walikwenda kuweka kambi nchini Uturuki lakini wachezaji walikwenda kwa mafungu, wengine wakaondolewa siku chache baada ya usajili (kipa Mbrazil) huku wachezaji wengine wakiungana na timu siku wiki moja kabla ya kuanza kwa ligi.

Haikutosha, Kocha wao wa wakati huo, Riobertinho aliiacha timu na kwenda nyumbani kwao Brazil na kuiacha timu chini ya msaidizi wake kabla ya kurejea tena siku chache kabla ya Ligi kuanza.

Aidha, Simba iliachana na wachezaji wake muhimu kama mshambuliaji Jean Baleke raia wa Congo aliyekuwa akiongoza kwa mabao kwenye timu hiyo akiwa na mabao nane pamoja na mshambuliaji wa Zambia Moses Phiri ambao walikuwa wakifanya vizuri ndani ya kikosi hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live