Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bila nembo ya NBC, klabu kushushwa daraja

NBC CUP Bila nembo ya NBC, klabu kushushwa daraja

Thu, 28 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MTENDAJI Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Almasi Kasongo amesema kuwa Klabu ambayo haitavaa nembo ya mdhamini NBC itashushwa daraja.

Kasongo amesema kuwa katika michezo ya mzunguko wa nne kumekuwa na baadhi ya timu zimevaa nembo hiyo huku nyingine zikishindwa kufanya hivyo kama inavyotakiwa kwa mujibu wa kanuni ya 16 (1) 7 ya Ligi Kuu Bara.

Baada ya kutokea hilo kamati imeagiza Klabu zote za NBC kuhakikisha zinavaa nembo yenye mdhamini mkuu kama ilivyoelekeza kwenye kanuni ya 16 (1.1), 16 (1.3), 16 (1.7) na 16 (1.8) ya Ligi Kuu kuhusu mdhamini.

Alieleza kuwa timu yoyote itakayoshindwa kufanya hivyo itatoza faini ya Sh3 milioni na kama makosa hayo yatakuwa yakijirudia itachukuliwa hatua kali zaidi ikiwemo kushushwa daraja.

Kasongo amesema kuwa agizo hilo linaanza kutekelezwa tangu tangazo limetoka Oktoba 27, huku akivitaka Klabu, wadau wote kwa maana ya viongozi, wachezaji na mashabiki kuzingatia kanuni hizo maana ndizo msahafu na muongozo wetu.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz