Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bila kulea Vipaji ngumu kutoboa

Vijana Kuwandaa Wachezaji wa Timu ya Taifa “Taifa Stars” waliopita kwenye Timu ya Vijana U17 iliyoshiriki AFCON U17

Tue, 16 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kila Mtanzania na mpenda soka ameona kilichotokea katika harakati zetu kama Taifa katika kutafuta nafasi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia Qatar 2022.

Tumepoteza nafasi hiyo na imechukuliwa na DR Congo, Timu ambayo imesheheni ubora katika kila eneo la kikosi chake.

Tulifanikiwa kutoa sare, ugenini dhidi yao kwa Mkapa tukafa goli 3-0.Kama taifa tumewekeza zaidi kwenye hamasa na si katika mipango endelevu na ya muda mrefu.

Huu ni muda wa Serikali kuwekeza kwa dhati kwenye michezo ili kupunguza idadi ya vijana wasio na kazi mtaani.

Tunatakiwa angalau kila mkoa uwe na Sports Academy kwa ajili ya kuwalea watoto wenye vipaji vya michezo kwenye misingi bora ambapo wengi tutawatoa nje taifa.

Kijana atakaekuzwa kwenye misingi bora ya michezo atakuwa na nidhamu kwenye maisha yake binafsi pamoja na uwanjani.

Binafsi naamini nchi hii ina vipaji vingi kwenye soka, ngumi, riadha, basketball na volleyball, hivyo ni siala la miundombinu ya kulea vipaji hivyo pamoja sera ya michezo.

Kilichotokea kwa Taifa Stars kuondolewa katika mbio za kuwaniwa kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2022 ni kwa kuwa tulizidiwa uwezo, ukitazama ubora wa wapinzani ulivyokuwa hasa DR Congo ni wazi kuwa ingekuwa ngumu kwetu ‘kutoboa’.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live