Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bila Kombe la AFCON, hakuna posho timu ya Taifa Sauzi

Afrique Du Sud Ethiopie 2 E1635848841636 768x493 1 Bila Kombe la AFCON, hakuna posho timu ya Taifa Sauzi

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika Kusini (SAFA) limekubaliana na wachezaji wa Timu ya Taifa hilo "Bafana Bafana" kwamba iwapo wasipofanikiwa kutwaa Taji la AFCON 2023 basi hawatopewa pesa yoyote Ile kama posho.

Pia wameambiwa iwapo watashinda basi watakabidhiwa kitita cha Tsh Bilioni 17 yote wagawane wenyewe kama ilivyosema sehemu ya kauli ya Raisi wa Shirikisho la Mpira (SAFA)

"Tunahitaji Kombe lije kwetu na tunao wachezaji wa kulileta. Haiwezekani wakiwa kwenye vilabu vyao binafsi wanajituma alafu wakija huku wanacheza kizembe. Tumekubaliana nao wakileta Kombe tunawapa $7m na wakilikosa basi hatutotoa kiasi chochote cha fedha." amesema Rais huyo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live