Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bigirimana wa Yanga afungua akaunti ya mabao Ulaya

Gael Bigirimana  Lindng Bigirimana wa Yanga afungua akaunti ya mabao Ulaya

Mon, 29 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa zamani wa Yanga SC, Gael Bigirimana amefungua akaunti ya mabao baada ya kuisaidia klabu yake ya Dungannon Swifts FC kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Linfield Ligi Kuu Northern Ireland.

Gael Bigirimana alifunga bao hilo mnamo dakika ya 62 ya mchezo huku bao la ushindi likafungwa na Dean Curry dakika ya 80 ya mchezo.

Kwasasa timu hiyo inakamata nafasi ya kumi kati ya timu kumi na mbili. Bao la kufutia machozi kwa upande wa Linfield lilifungwa na mchezaji Matthew dakika ya 51.

Mbali ya kuitumikia timu ya Yanga SC, Gael Bigirimana amewahi kukipiga katika vilabu vya Newcastle United, Rangers, Coventry City, Hibernian, Motherwell, Solihul Glentora na Dungannon.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live