Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bigirimana arejea Yanga kimyakimya

IMG 20230729 WA0009 Bigirimana arejea Yanga kimyakimya

Sat, 29 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Kiungo wa Yanga, Gael Bigirimana raia wa Burundi bado yupo kwenye Kambi ya timu hiyo katika viunga vya Avic Town, Kigamboni Dar es Salaam.

Bigirimana ambaye amewahi kuichezea Ligi Kuu ya Uingereza akiitumikia Newcastle United, alijiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu uliopita akiwa mchezaji huru lakini hakuonyesha kiwango cha kuwaridhisha Wananchi chini ya Kocha Nasreddine Nabi.

Katika dirisha dogo la msimu huo, Yanga walimtema Mrundi huyo huku ikifaiwa kuwa alikuwa akiidai klabu hiyo kiasi cha Tsh milioni 700 ambapo uongozi wa Yanga ulikubaliana naye kuwa atalipwa kwa mafungu.

Kwa sasa inaonekana Bigirimana amerejea tena kikosini, ambapo inasemekana anaishi kambini hapo na kulipwa na mshahara na Klabu ya Yanga na anajumuika na wenzake kwenye mazoezi kama kawaida.

Mpaka sasa uongozi wa Yanga haujatoa tamko lolote kuhusu mchezaji huyo mwenye wasifu mkubwa Afrika Mashariki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live