Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bifu la Solskjaer, Ronaldo ni hivi

Ole G Solkjaer Bifu la Solskjaer, Ronaldo ni hivi

Sun, 10 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa zamani wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amefunguka juu ya kile kilichotokea kati yake na mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Cristiano Ronaldo wakati wote wapo kwenye timu hiyo.

Ronaldo ambaye alisajiliwa mwaka 2021 kwa ajili ya kuboresha zaidi safu ya ushambuliaji ya Manchester United alikuwa sehemu kundi jipya la mastaa walioingia kwenye timu hiyo kipindi hicho akiungana na Raphael Varane na Jadon Sancho.

Kwenye mchezo wake wa kwanza alifunga mabao mawili dhidi ya Newcastle kisha akafunga tena dhidi ya West Ham.

Baada ya kuanza vizuri kiasi hicho akacheza tena mechi na Aston Villa na baada ya hapo Solskjaer anasema Ronaldo mwenyewe aliomba kupumzishwa na yeye akafanya hivyo kwa kumweka benchi.

Hata hivyo, Solskjaer anaeleza alishangazwa na kitendo cha Ronaldo kuchukia kukaa benchi kwa sababu lilikuwa ni ombi lake mwenyewe.

Licha ya hayo yote Solskjaer anaelezayeye ndiye aliyekubali kusajiliwa kwa staa huyo kutokana na ile hali yake ya kupambana lakini mwisho mambo yakawa tofauti.

Anaeleza kwake yeye bado anamheshimu Ronaldo na bado anaamini ni mchezaji mwenye nidhamu kubwa licha ya yote yaliyotokea.

“Nilipokuwa kocha wa Manchester United,sikumbuki matatizo ambayo Ronaldo aliyasababisha kwenye timu, zaidi ya mechi dhidi ya Everton ambapo aliamua kuondoka kabisa uwanjani baada ya kufanyiwa mabadiliko. Nilikuwa na uhusiano mzuri nayeye na nafikiria alikuwa na adabu hata pale na alikuwa amekwazika.”

Kwa upande wa Ronaldo kwenye mahojiano yake na Piress Morgan aliwahi kuweka wazi hakuwahi kumheshimu Solskjaer kwa sababu yeye hakuwa anampa heshima yake.

Chanzo: Mwanaspoti