Mzozo kati ya Kocha Marc Brys na Shirikisho la soka la Cameroon Fécafoot linaloongozwa na Samwel Eto’o umeonekana kufukuta tena baada ya afisa habari wa Shirikisho hilo kutuma wito kwa Kocha raia wa Ubelgiji kukabidhi Pasipoti za wachezaji kwa waratibu walioteuliwa na Samuel Eto’o.
Katika mkutano na Waandishi wa habari kocha Marc Brys alithibitisha kwamba uwanja wa Roumde Adjia ulitimiza masharti yote muhimu kwa mechi licha ya Shirikisho kuukataa Uwanja huo.
Fécafoot ilikuwa imechagua Mji wa Douala, lakini Marc Brys alipendelea Uwanja wa Yaoundé, ambapo baadae wachezaji wote walikubaliana na mkufunzi huyo katika mchezo dhidi ya Namibia.
Katika mchezo ambao ulipigwa kwa siku ya jana Septemba 7, Cameroon iliweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namibia mechi ya kufuzu kwa AFCON 2025 bao ambalo lilifungwa na mchezaji Vincent Aboubakar dakika ya 65.