Sat, 23 Oct 2021
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Wawakilishi wa Tanzania katika Mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, timu ya Biashara United ya Mara imekwama kwenda Libya kwa ajili ya mchezo wa marudiano Raundi ya pili Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji Al Ahli Tripoli uliopangwa kufanyika Oktoba 23, Jijini Benghazi.
Biashara United iliyoshinda 2-0 kwenye mechi ya kwanza Jumamosi iliyopita Dar es Salaam imekwama kuondoka hadi leo kutokana na changamoto za usafiri wa anga na sasa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linawasiliana na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mechi hiyo isogezwe mbele.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live