Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biashara yafanya biashara ya faida Djibouti

WANAJESHI WA MPAKANI Kikosi cha Biashara United

Fri, 10 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Biashara United maarufu kama "wanajeshi wa mpakani" hii leo wameonyesha maajabu baada ya kuibuka na ushindi katika mchezo wao wa awali wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Klabu ya Bishara imeibuka na Ushindi wa goli 1-0 dhidi ya klabu ya FC Dikhil ya nchini Djibout katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Stade du Ville.Goli hilo la ushindi la Biashara limefungwa na Denis Nkane 52'.

Lakini kilichowashangaza wengi sio ushindi bali namna ambavyo klabu ya Biashara imeyapitia mpaka kufika nchini Djibout.

Biashara imeondoka alfajiri ya leo Jijini Dar es Salaam kuelekea nchini Djibout na wamefika leo hii hii na wamecheza mechi hiyo ya mkondo wa kwanza na kuibuka na ushindi.

Wengi walikua na Mashaka kwa namna maandalizi waliyoyafanya kuwa hafifu huku ikisemekana baadhi ya wachezaji hawakua na hati za kusafiria.

Biashara itarudi nchini kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya mkondo wa pili ambayo watacheza jijini Dar es Salaam.

Hii ni mara ya kwanza kwa Biashara kushiriki Michuano ya Kimataifa tangu wapande daraja kucheza Ligi kuu, nafasi hii wameipata baada ya kumaliza nafasi ya nne msimu uliopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live