Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biashara United yatamba kurudi na nguvu mpya

Pamba Jiji FC Promoted Biashara United yatamba kurudi na nguvu mpya

Wed, 19 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kushindwa kupanda Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kufungwa jumla ya mabao 2-1 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa mikondo miwili ya 'play off', Klabu ya Biashara United imekubali yaishe, ikiahidi itarudi na nguvu mpya msimu ujao.

Katika salamu zake za shukurani kwa wadau mbalimbali baada ya kumaliza msimu, Rais wa Klabu hiyo jana, Gabriel Rugumila alisema kila mmoja katika nafasi yake alifanya kazi nzuri, wakiwamo wachezaji na benchi la ufundi, lakini mwisho wa siku hawakupata kile walichokihitaji na wameumizwa mno, lakini akaahidi kurejea msimu ujao na nguvu mpya.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Juni 2, mwaka huu, Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara, Biashara United ilishinda bao 1-0, kabla ya kufungwa mbaao 2-0, Jumapili, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi na kuzima ndoto zao za kutaka kurejea Ligi Kuu mara ya kwanza baada ya kushuka msimu wa 2021/22.

"Tumeipigania timu yetu mpaka jasho la mwisho, tunashukuru kumaliza msimu salama, tunalishukuru benchi la ufundi likiongozwa na Amani Josiah, Edna Lema na Ivo Mapunda ambao walifanya kazi nzuri, wakiwamo wachezaji wetu wote ambao wameitumikia timu kwa uaminifu mkubwa, lakini wameumizwa na matokeo ya mwisho na sisi pia tumeumia, ila matumaini yetu ni kujipanga kwa msimu ujao, tutarudi na nguvu mpya," alisema rais huyo.

Rugumila pia alimshukuru Mkuu wa Mkoa aliyeondoka, Said Mtanda ambaye kwa sasa amehamia Mwanza, pamoja na aliyekuwapo sasa kwenye mkoa wa Mara wa sasa, Venance Mtambi, wabunge na wafanyabiashara, pamoja na mashabiki kwa kujitolea kwao.

Baada ya kumaliza nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi ya Champinship, Biashara United iliifunga Mbeya Kwanza katika mchezo wa kwanza wa 'play off' jumla ya mabao 4-0, ikishinda 2-0 nyumbani na ugenini, kabla ya kukutana na kigingi, Tabora United.

Matokeo ya mechi ya Jumapili yamezifanya timu hizo kila moja kusailia ilikokuwa, Tabora United ikibaki Ligi Kuu na Biashara United nayo Ligi ya Champoinship.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live