Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biashara United yakana kupokea rushwa

BIASHARAAA Timu ya Biashara United

Tue, 26 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Biashara United umekanusha uvumi unaosambaa mitandaoni kuhusu viongozi wao kupokea rushwa kutoka timu ya Al Ahly Tripoli ili kukwamisha safari yao kuelekea nchini Libya kwa ajili mechi ya marudiano kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Biashara United inasubiri maamuzi ya CAF juu ya hatma ya mchezo wao ambao haukuchezwa baada ya wawakilishi hao kushindwa kufika uwanjani nchini Libya kwa sababu ya kukosa vibali vya ndege.

Kwa sasa biashara imesafiri kuelekea Sumbawanga kwa ajili ya mchezo wao na Timu ya Tanzania Prisons.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live