Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biashara United yakaa mguu sawa Bara

Biashara Unitedd Biashara United yakaa mguu sawa Bara

Fri, 7 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati ikisubiri kumjua mpinzani wake kwenye mchezo wa mtoano kucheza Ligi Kuu, Biashara United imeanza kujifua kuweka utimamu, mbinu na saikolojia sawa ili kuwa tayari kwa pambano hilo.

Biashara United itacheza na timu itakayopoteza mchezo wa mtoano kati ya JKT Tanzania na Tabora United na katika mchezo wa kwanza uliochezwa Jumatatu kwenye Uwanja wa Alli Hassan Mwinyi, Tabora, maafande hao walishinda kwa mabao 4-0.

Timu hizo zitarudiana kesho Uwanja wa Meja Jenerali Isamhuyo, Dar es Salaam huku mshindi akibaki Ligi Kuu na itakayopoteza itacheza mchezo wa kwanza na Biashara United Juni 12 Uwanja wa Karume, Musoma na kurudiana Juni 16.

Kocha Mkuu wa Biashara United, Amani Josiah alisema wameanza maandalizi wiki hii wakianza na mazoezi ya viungo (Gym) kuimarisha utimamu wa mwili, kisha watakwenda uwanjani na darasani kuboresha mbinu zao kwa sababu wanafahamu wanakutana na mpinzani mgumu na mzoefu zaidi yao.

Alisema mchezo huo utakuwa mgumu kwakuwa zinakutana timu zenye madaraja tofauti ndiyo maana wanafanya mazoezi magumu ili washinde, huku akitamba siyo jambo geni kwao kwani inawezekana kama watafanya maandalizi ambayo yatawafanya waamini wana kitu cha kujivunia.

“Tumeanza na utimamu wa mwili tutaenda uwanjani na baadae darasani tunashukuru uongozi kwa kusapoti programu hizi, hii yote ni kuona namna ambavyo tunaweza kufanya vizuri tunakwenda kucheza na timu ya Ligi Kuu lazima na sisi tujiimarishe kila eneo,” alisema Josiah.

“Wachezaji wameitikia maandalizi yetu wanafurahia programu tulizonazo na wanazitekeleza, kwa hiyo naamini baada ya muda tutajizatiti tukisubiri kufahamu mpinzani wetu lakini tuwe katika kiwango ambacho ni kizuri linapokuja suala la utimamu, mbinu na saikolojia,” alisema.

Chanzo: Mwanaspoti