Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biashara United wanaitaka timu yoyote Ligi Kuu

Wstfdtqfwtdd Biashara United wanaitaka timu yoyote Ligi Kuu

Tue, 28 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

‘Aje yeyote’. Ni kauli na tambo za Biashara United ikieleza kuwa tayari kukabiliana na mpinzani yeyote wa Ligi Kuu katika mchezo wa mchujo (play off) kutafuta kupanda Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Biashara United ina uwezekano wa kukutana kati ya Kagera Sugar na Tabora United ambazo zipo nafasi ya 13 na 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu hadi sasa ikiwa imebaki mchezo mmoja kumaliza msimu.

Hii ni baada ya timu hiyo kushinda kwa jumla ya mabao 4-0 katika michezo miwili ya mtoano nyumbani na ugenini dhidi ya Mbeya Kwanza katika Ligi ya Championship.

Mkurugenzi wa bodi ya timu hiyo, Agustine Mgendi amesema baada ya kufanya kweli kwenye michezo hiyo kwa sasa wanasubiri mpinzani yeyote na kwamba wachezaji watabaki kambini kusubiri mpinzani.

Ametamba kuwa malengo yao ilikuwa kupanda Ligi Kuu moja kwa moja bila kusubiri Play off, lakini kutokana na kushindwa sasa wanasubiri nafasi hiyo na kwamba msimu ujao lazima warudi tena Ligi Kuu.

“Sisi tulikuwa tupande moja kwa moja lakini haikuwezekana kwa sababu zilizoonekana, hivyo kilichobaki ni kupitia nafasi hii na tunamsubiri yeyote kuweza kufikia malengo yetu,” amesema Mgendi.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Aman Josiah amesema wataendelea kuwaandaa vyama wachezaji kiufundi na kisaikolojia ili kuhakikisha wanatimiza malengo na kurejesha heshima ya Biashara United.

“Tunaendelea na program kujiandaa na yeyote kwa sababu haijajulikana, niwapongeze wachezaji kwa kujituma na kuwashukuru viongozi kwa ushirikiano, sisi benchi la ufundi tunaenda kujipanga na yeyote,” amesema.

"Tutawafuatilia wapinzani katika mechi zao za 'play off' kuwasoma udhaifu wao, lakini tutaangalia uwezekano wa kuwa na mechi kadhaa za kirafiki ili kutengeneza utimamu kwa wachezaji wetu."

Chanzo: Mwanaspoti