Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biashara United mguu mmoja Ligi Kuu

Biashara United Championship Biashara United.

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Biashara United sasa italazimika kusaka matokeo ya jumla kwenye michezo yake miwili dhidi ya itakayotoka Ligi Kuu kucheza 'Play Off' ili kupanda daraja.

Biashara juzi ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya Kwanza kwenye mchezo wa pili wa mchujo kuwania kupanda daraja msimu ujao na kucheza Ligi Kuu.

Ikicheza ugenini, Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara ambako Mbeya Kwanza inautumia kama uwanja wake wa nyumbani, Biashara United ilipata mabao yake mawili kupitia kwa Herbert Lukindo na Abeid Athumani.

Ilikuwa ni mechi ya mkondo wa pili, baada ya awali kushinda pia mabao 2-0 nyumbani, Uwanja wa Karume, Musoma, mkoani Mara, mchezo uliochezwa Mei 19, wafungaji wakiwa ni Abeid na Boban Zirintusa, hivyo kufanikiwa kupita kwenye hatua hiyo ya mchujo kwa jumla ya mabao 4-0.

Timu hiyo iliyoshuka daraja kutoka Ligi Kuu msimu wa 2021/22, sasa itasubiri mshindi kati timu zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14 kwenye Ligi Kuu.

Timu hizo za Ligi Kuu zitacheza mechi ya mchujo ambapo mshindi wa jumla atabaki, na itakayofungwa itakwenda kucheza mechi ya 'play off' na Biashara United.

Biashara na Mbeya Kwanza, zililazimika kucheza mchujo, baada ya kumaliza nafasi ya tatu na ya nne katika Ligi ya Championship.

Mbeya Kwanza ilimaliza nafasi ya tatu na pointi zake 65, Biashara United ikiwa ya nne, ilikusanya pointi 62 huku ikiziacha timu za KenGold na Pamba zikipanda Ligi Kuu moja kwa moja.

Msimu uliopita, Mashujaa FC, ilipanda Ligi Kuu kwa kushinda mechi yake ya 'Play off' dhidi ya Mbeya City ambayo ililazimika kucheza mchezo huo baada ya kufungwa na KMC katika michezo miwili ya mchujo, nyumbani na ugenini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live