Kocha mkuu wa Real Madrid Carlo Ancelotti anatumaini kuwa Karim Benzema atakuwa fiti kuichezea Real Madrid katika fainali ya Kombe la Dunia la Vilabu.
Benzema ambaye ni mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or mwaka jana hakwenda Morocco mapema wiki hii kwa ajili ya michuano hiyo, baada ya kupata jeraha la misuli ya paja.
Hata hivyo, Ancelotti alithibitisha baada ya Madrid kuishinda Al Ahly 4-1 katika nusu fainali hapo jana na kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 atasafiri kwenda kufanya mazoezi na wachezaji wenzake siku ya kesho.
Benzema ataungana na Eder Militao, ingawa Ancelotti ambaye alithibitisha Marco Asensio na Dani Carvajal waliwekwa benchi dhidi ya Al Ahly kutokana na matatizo ya utimamu wao bado anatia shaka zaidi uwezekano wa beki huyo kumenyana na Al-Hilal siku ya Jumamosi.
Kocha huyo amesema kuwa; “Hawajapona kabisa, Karim anaendelea vizuri na kuna mashaka zaidi kuhusu Militao ila watafanya mazoezi siku ya kesho halafu tutaona. Carvajal alikuwa na homa na Asensio alizidiwa kidogo. Nadhani atakuwa tayari kwa Jumamosi.”
Madrid wanaenda kunyakua taji la tano la Klabu Bingwa ya Dunia, na mafanikio yao ya kwanza yalikuja chini ya Ancelotti nchini Morocco mnamo Desemba 2014.
Timu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia iliwashangaza mabingwa wa Copa Libertadores Flamengo kwa kichapa mabao 3-2 siku ya Jumanne, na Ancelotti alikiri kushangazwa na matokeo hayo.
Alisema: “Nilishangaa. Katika ngazi ya mtu binafsi Flamengo walikuwa na faida, lakini wako katika maandalizi ya msimu mpya na kiwango chao cha kimwili si cha juu, kama timu nyinginezo.”