Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benzema hati hati kuikosa El Classico

Fbl Eur C1 Real Madrid Shakhtar 1 Mshambuliaji wa Madrid Karim Benzema na Kocha wake Carlo Ancelotti

Tue, 15 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti ameonesha kutokuwa na wasiwasi kwa mshambuliaji Karim Benzema licha ya mchezaji huyo kupata jeraha dogo baada ya kufunga bao lake la pili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Real Mallorca siku ya Jumatatu.

Benzema aliweka mbili katia ushindi huo na bao lingine likiwekwa kambani na mchezaji Vinicius Jr lakini alionekana kama kuumia wakati wa kushangilia baada ya kufunga bao la tatu.

Madrid walilazimika kucheza na watu 10 baada ya Benzema kupata tatizo sababu walikuwa tayari wametumia wachezaji wote watano wa akiba na Ancelotti alisema kwamba wanasubiri kuonakama tatizo lina ukubwa kiasi gani.

“Lazima tumtathmini katika siku chache zijazo – mambo hayaonekani kuwa mabaya sana,” Ancelotti alisema.

“Karim hakujisikia vizuri baada ya kurukaruka – tunapaswa kusubiri hadi Jumatano ili kujua zaidi.”

Benzema tayari amefunga mabao 22 katika michezo 25 LaLiga msimu huu na Real Madrid wapo juu kwa alama 10 mbele ya Sevilla ambao wanashika nafasi ya pili na shaka ipo kwa Benzema kuelekea mechi ya mahismu wao wa LaLiga Barcelona siku ya Jumapili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live