Straika wa Real Madrid, Karim Benzema ameripotiwa kuwa majeruhi na kuibua wasiwasi kwamba huenda akakosa mechi ya marudiano ya hatua ya 16 bora kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool.
Straika wa Real Madrid, Karim Benzema ameripotiwa kuwa majeruhi na kuibua wasiwasi kwamba huenda akakosa mechi ya marudiano ya hatua ya 16 bora kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool. Staa huyo alifunga mara mbili kwenye kipindi cha pili katika mechi ya kwanza iliyofanyika uwanjani Anfield, ambapo Real Madrid ilishinda 5-2. Benzema ni mchezaji muhimu katika mafanikio ya Real Madrid linapokuja soka la Ulaya miaka ya karibuni.