Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benzema awaondosha Chelsea UEFA

Karim Benzema Mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema akifunga bao lililowaondosha mabingwa watetezi Chelsea

Wed, 13 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wababe wa Ulaya, Real Madrid wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya kuchapwa mabao 3-2 na waliokuwa mabingwa watetezi, Chelsea usiku wa jana Uwanja wa Santiago Bernabéu Jijini Madrid, Hispania.

Mabao ya Chelsea yalifungwa na Mason Mount dakika ya 15, Antonio Rudiger dakika ya 51 na Timo Werner dakika ya 75, wakati ya Real Madrid yalifungwa na Rodrygo dakika ya 80 na Karim Benzema dakika ya 96.

Baada ya The Blues kumaliza wanaongoza 3-1, mechi iliongezewa dakika 30, kwa sababu matokeo ya jumla yalikuwa 4-4.

Real wanakwenda Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 5-4 baada ya kuwachapa mabingwa hao wa msimu uliopita 3-1 kwenye mechi ya kwanza Jumatano iliyopita Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London, huku magoli yote yakiwekwa kimiani na Karim Benzema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live