Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benzema ataja timu atakaystaafia Soka

Karim Benzema Winner Mshindi wa Tuzo ya Ballon D'or 2022

Tue, 18 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa klabu ya Real Madrid na timu ya Taifa ya Ufaransa Karim Benzema, amesema anapanga kustaafia Madrid kwa kuwa haoni nafasi ya kwenda mahala pengine.

Staa huyo mshindi wa tuzo ya Ballon D'or amezungumza hayo katika hafla ya ugawaji wa tuzo hizo jana usiku wakati akiibuka mshindi wa tuzo hiyo pale alipoulizwa na mwandishi wa habari kuhusu hatma yake ndani ya klabu hiyo.

“Nimepanga kustaafu hapa Real Madrid. Hakuna sehemu nyingine ninayoweza kustaafia ndivyo nionavyo mimi” Alisema Karim Benzema.

Staa huyo ambaye anashikilia kiatu cha mfungaji bora wa ligi kuu ya Hispania pamoja na ligi ya mabingwa ulaya tayari amefikisha miaka 14 ndani ya klabu hiyo amepanga kumalizia soka lake kwenye klabu hiyo ambayo amefanikiwa kushinda mataji mbalimbali ndani ya klabu hiyo.

Karim Benzema anaona klabu hiyo hiyo kama sehemu pekee ya kumalizia soka lake kwasababu ndio klabu kubwa kabisa duniani hivo haoni kama kuna sehemu nyingine atakwenda baada ya Real Madrid ikawa na ukubwa zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live