Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benzema ampiku Henry, na kumkaribia Raul Bernabeu

Karim Benzema Real Karim Benzema akishangilia moja kati ya magoli mawili aliyofunga dhidi ya Mallorca

Tue, 15 Mar 2022 Chanzo: eatv.tv

Baada ya nyota wa Real Madrid Karim Benzema kufunga mabao mawili kati ya matatu yaliyowapa ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Mallorca jana usiku na kufanya vinara hao wa La Liga kuendeleza kujiimarisha kileleni kwa tofauti ya alama 10, alama 66 mbele ya Sevilla wenye alama 56 nafasi ya pili.

Mabao hayo mawili ya Benzema yalikuwa mabao yake namba 31 na 32 kwa msimu huu aliyofunga katika mashindano yote, na amefikisha magoli 22 ya ligi kuu ya hisapnia La Liga Santender msimu huu na akiwa ametoa pasi 11 za magoli.

Takwimu hizo sasa zinamfanya Karim Benzema kuwa amefunga idadi kubwa zaidi ya magoli katika msimu mmoja tangu alipofanya hivyo msimu wa mwaka 2011 /12 alipomaliza msimu na magoli 32.

Pia magoli hayo yamemfanya Benzema kufikisha jumla ya magoli 311 aliyoifungia klabu yake ya Real madrid, na hivyo kuanza kuikaribia rekodi ya gwiji wa zamnai wa miamba hiyo ya La Liga Raul Gonzalez ambaye ndio mfungaji bora wa muda wote wa Los Blancos hadi sasa akiwa amefunga mabao 323.

Vili vile kwa magoli hayo mawili Benzema kwa sasa ndiyo amekua mfungaji bora wa muda wote kutoka nchini Ufaransa, akiwa amefikisha jumla ya mabao 413 akiipiku rekodi ya muda mrefu ya Gwiji wa zamani wa nchi hiyo Thierry Henry aliyefunga mabao 411.

Chanzo: eatv.tv