Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benzema amfungulia Mashtaka Waziri wa Ufaransa

Benzema With Damian.png Benzema amfungulia Mashtaka Waziri wa Ufaransa

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa ‘klabu’ ya Al-Ittihad kutoka nchini Saudi Arabia, Karim Benzema amemfungulia mashitaka Waziri wa Mambo ya Ndani Ufaransa Gerald Darmanin kwa kumchafulia jina.

Hii inakuja baada ya Benzema ku-share ujumbe kupitia ukurasa wake wa X kuwa anaunga mkono watu wa Gaza ambapo Darmanin kutokana na post hiyo alinukuliwa akisema kuwa Benzema anaushirikiano na kundi la Muslim Brotherhood ambalo limepigwa marufuku katika baadhi ya nchi.

Benzema alikanusha tuhuma hizo huku akieleza kuwa umaarufu wake unatumiwa vibaya katika mambo ya Siasa.

Hii siyo mara ya kwanza kwa Waziri Darmanin kumshutumu Benzema, aliwahi kudai kuwa mshambuliaji huyo aligoma kuimba wimbo wa Taifa alipokuwa akijiandaa na ‘mechi’ ya ‘timu’ ya Ufaransa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live