Waziri wa Mambo ya ndani wa nchini Ufaransa, Gerald Darmanin, anamshutumu mchezaji wa ‘klabu’ ya Al-Ittihad ya Uarabuni, Karim Benzema kwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Muslim Brotherhood, baada ya kiungo huyo, kuonesha kuunga mkono Taifa la Palestina katika mzozo wao na Israel, siku za hivi karibuni.
Inadaiwa kuwa Benzema alitumia ukurasa wake wa Twitter kuandika ujumbe ambao aliwataka watu waiombee Palestina na raia wake walio kuwa waathirika wa milipuko dhidi ya Israel.
Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali inadaiwa baada ya ujumbe huo, mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid, alipokea ukosoaji mkubwa kutoka kwa watu mbalimbali akiwemo waziri huyo.