Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benzema afukuzwa mazoezini

Kante Benzema.jpeg Benzema afukuzwa mazoezini

Fri, 9 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Tetesi za mshambuliaji wa Al Ittihad, Karim Benzema kuondoka kwenye timu hiyo zimezidi kupamba moto baada ya staa huyo mwenye umri wa miaka 36, kufukuzwa mazoezini na kocha wake Marcelo Gallardo.

Benzema aliwasili mazoezini Jumatatu ya wiki hii kujiunga na timu ikiwa ni baada ya kuachwa kwenye kikosi kilichoingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu.

Inadaiwa kuwa Benzema alichelewa kurudi kwenye mapumziko ya siku 17 ambayo wachezaji wote walipewa na hakuwa anapatikana kwenye simu kwa sababu nchini Mauritius alikoenda kula bata kulikuwa na shida ya mtandao.

Aliporejea alishindwa kutoa maelezo ya kumshawishi kocha wake ambaye alimtaka kutofanya mazoezi na wenzake na badala yake afanye mwenyewe katika kipindi hiki ambcho ishu yake haijapatiwa ufumbuzi.

Badala ya kufuata maagizo ya kocha, Benzema aliamua kuondoka kabisa mazoezini na akaonekana tena siku iliyofuatia akifanya mazoezi na wachezaji waliotoka kwenye majeraha. Hiyo imesababisha asicheze mechi ya jana ya Ligi Kuu nchini Saudi Arabua dhidi ya Al-Tai ambapo Ittihad ilishinda mabao 3-0.

Hadi sasa haijajulikana ikiwa staa huyu aliyesajiliwa mwaka jana ataondoka kwenye timu hiyo ama atabaki ingawa Manchester United na Chelsea zinahusishwa naye.

Chanzo: Mwanaspoti