Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benzema Mfaransa wa kwanza kunyakua Ballon d'Or baada ya Zidane

Benzema Ballon 1.jpeg Benzema

Tue, 18 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Karim Benzema ameshinda tuzo ya Ballon d'Or kwa mara ya kwanza, baada ya kuwa na mwaka bora wa 2022 akiwa Real Madrid.

Benzema aliibeba miamba hiyo ya Uhispania kushinda Mataji ndani ndani na Kimataifa kwa msimu wa 2021/22.

Benzema alifunga mabao 44 na kusaidia 15 katika mechi 46 katika michuano yote akiwa na Madrid, akiwa na wastani wa mchango wa mabao kila baada ya dakika 66.4 huku klabu hiyo ikishinda La Liga na kombe la UEFA Champions League.

Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 34 alifunga magoli 15 kwenye #UCL pekee huku 10 kati ya hayo akifunga katika hatua ya mtoano. Kiwango chake katika Ligi ya Mabingwa Ulaya ndicho kimechangia kwa kiasi kikubwa kuwa mshindi anayestahili wa tuzo ya Ballon d'Or 2022.

Hat-trick yake ya kushangaza dhidi ya PSG, Real Madrid ikipindua meza kibabe kwa ushindi wa jumla wa 3-2 kufuatia kipigo cha 1-0 ugenini sambamba na mabao matatu katika mechi mbili za nusu fainali dhidi ya Manchester City imekuwa chachu ya mafanikio yake kwa msimu wa 2021/22.

Benzema amekuwa mchezaji wa kwanza wa Ufaransa kushinda Ballon d'Or tangu Zinedine Zidane.

Benzema 2022 akiwa umri wa miaka 34 na miezi 10 ni mchezaji wa pili Mkongwe zaidi kutwaa tuzo hiyo baada ya Stanley Matthews miaka 41 na miezi 10 mnamo 1956.

Rekodi ya Stanley Matthews ya kutwaa tuzo hiyo akiwa na umri huo huenda ikachukua muda mrefu kuvunjwa au ikadumu milele labda kama Cristiano Ronaldo atakuwa na msimu bora wa 2027/27.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live