Real Madrid imewapa mkono wa kwaheri nyota wake wanne waliothibitika kuondoka ndani ya miamba hiyo baada ya kuitumikia kwa mafanikio makubwa
Nahodha Karim Benzema ataenda kujiunga kwenye ligi kuu soka ya Saudi Arabia juma lijalo, huku Marco Asensio akisaini mkataba wa awali na PSG kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika
Mariano Diaz naye ameruhusiwa kuondoka kama mchezaji huru baada ya kumalizika mkataba wake huku Eden Hazard akifikia makubaliano ya kuvunja mkataba na miamba hiyo baada ya kushindwa kuonesha makali yake tangu ajiunge kutokea Chelsea na sasa ni mchezaji huru.
Beki mzawa wa klabu hiyo Nacho Fernandez bado hajaamua kuongeza mkataba na anasubiri kujua hatma yake juma lijalo kwani Inter Milan wametangaza nia ya kuhitaji huduma yake lakini watazungumza naye baada ya fainali ya ligi ya mabingwa.