Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benoit Ekotto: Nilikuwa nacheza mpira nipate pesa sio kwa mapenzi

Benoit AssouEkotto Ottenham Vs Watford 2811202 Mchezaji wa zamani wa klabu ya Tottenham na timu ya Taifa ya Cameroon Benoit Ekotto

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Tottenham na timu ya Taifa ya Cameroon Benoit Ekotto ameeleza kuwa kwake mpira ulikuwa kazi na sio mapenzi kama wengine wanavyodai.

"Watu wote wakienda kazini, ni kwa ajili ya pesa.Kwa hiyo huwa sielewi kwanini nikisema nacheza kwa ajili ya pesa watu wanashtuka.Sisemi kuwa nauchukia mpira lakini sio kitu ninachokipenda."

"Wachezaji wengine watakubaliana na mimi .Nina uhakika kwa asilimia 200, sikiliza wakala wako akikupigia na kukuambia nina klabu kwa ajili yako swali la kwanza ni kiasi gani? Ni biashara."

"Sidhani kama inasaidia kwa mimi kuwa mkweli lakini ni nzuri kibiashara kusema 'naipenda klabu, nawapenda mashabiki, blah blah blah,.... Mimi siko hivyo."

-Benoit Assou-Ekotto, nyota wa timu ya Taifa ya Cameroon.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live