Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki za PBZ, Said Said ameikabidhi kamati ya maandalizi ya Kombe la Mapinduzi mwaka 2024 vifaa vya michezo ikiwa ni sehemu ya udhamini wake katika kombe hilo.
Vifaa hivyo vimepokelewa na Mwenyekiti wa Kombe la Mapinduzi, Mbarouk Othman, wengine waliokuwepo kwenye makabidhiano hayo ni pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya kombe la Mapinduzi, Khalid Hamrani, Mkurugenzi wa Biashara wa PBZ, Eddie Mhina na Mkuu wa Kitengo cha Usaidizi kwa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, Harith Fentu.
PBZ pamoja na kuwa mdau kwenye tasnia ya michezo ikiwa kama ni mdhamini mkuu wa Ligi ya Soka ya Zanzibar (PBZ Premier League) pia imekuwa mstari wa mbele kwenye kuchangia shughuli mbalimbali za michezo.