Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benjamin Moukandjo atundika daruga

Benjamin Moukandjo Benjamin Moukandjo

Tue, 15 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Cameroon, Benjamin Moukandjo ametangaza kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 34.

Moukandjo aliwahi kuwa nahodha wa Timu ya Taifa ya Cameroon hadi wanapotwaa Kombe lao la tano la Kombe la Mataifa ya Afrika 2017 nchini Gabon.

Alistaafu kuichezea timu ya taifa mwaka wa 2018 baada ya kocha wa wakati huo Clarence Seedorf kusema “wachezaji wazuri hawawezi kucheza China au Asia.

Nyota huyo ambaye anachaza nafasi ya kiungo aliwahi kucheza katika klabu mbalimbali kama vile, AS Nancy-Lorraine, FC Lorient, Nimes Olympique, Stade Reims zote za Ufaransa, Beijing Hongdeng F.C ya China, AS Monaco ya Ufaransa, Jiangsu FC ya China, AE Larisa ya Ugiriki, RC Lens ya Ufaransa na Valenciennes FC ya Ufaransa.

Kwa ujumla katika vilabu hivyo, amecheza mechi 302 akifunga mabao 84 na kufanikiwa kutoa asisti 21. Katika maisha yake ya Soka amepata kadi za njano 30 na kadi moja tu nyekundu.

Moukandjo unaweza kusema hakuwa mchezaji wa makombe, katika vilabu hivyo hakuna klabu hata moja aliyofanikiwa nayo na kutwaa kikombe, zaidi ya Timu ya Taifa ya Cameroon mwaka 2017 na ndio Kombe pekee alilofanikiwa kuwa nalo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live