Mlinzi wa Manchester City Benjamin Mendy amefungiliwa mashitaka ya ubakaji na unyanyasaji wa kingono kwa mabinti wenye umri wa miaka 16 na idadi ya mashitaka imezidi kuongezeka na kufikia mashitaka sita
Mendy amekuwa kizuizini tokea mwezi agosti alipokamatwa na rufaa zake kadhaa alizowasilisha kukataliwa na jaji, kwa sasa anamashitaka sita kwa makosa aliyoyafanya kati ya mwezi oktoba 2020 mpaka agosti 2021.
Mendy kwa sasa yupo rumande anasubilia kusomewa mashitaka yake kwenye Mahakama ya Stockport mjini Liverpool siku ya jumatano huku hukumu ya kesi zake ikitarajiwa kutoka tarehe 24 jamuari 2022.
Benjamin Mendy alisajiriwa na klabu ya Manchester City mwaka 2017 akitokea Monaco kwa ada ya uhamisho Pauni milioni 52, lakini tokea ashutumiwe kwa makosa ya ubakaji klabu ya Manchester City imemsimamisha ili kupisha uchunguzi mpaka hapo atakapo kutwa hana hatia.