Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benjamin Mendy kuipeleka Manchester City mahakamani

Benjamin Mendy Kuipeleka Manchester City Mahakamani Benjamin Mendy kuipeleka Manchester City mahakamani

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Benjamin Mendy anaipeleka klabu yake ya zamani ya Manchester City kwenye mahakama ya ajira kuhusu zaidi ya mamilioni ya pauni anazodai kukatwa kwa mishahara bila ruhusa yake.

Beki huyo wa pembeni wa Ufaransa Mendy, 29, aliondoka City mwishoni mwa kandarasi yake msimu huu wa joto.

Aliondolewa mashtaka kadhaa ya ubakaji na jaribio la ubakaji dhidi yake.

Inadaiwa City iliacha kumlipa Mendy Septemba 2021 baada ya kufunguliwa mashtaka na kuwekwa kizuizini.

Katika taarifa yake, ilithibitishwa kuwa wakili mkuu wa masuala ya michezo nchini Uingereza Nick De Marco anashughulikia kesi ya Mendy, ambayo ni sawa na "madai ya mamilioni ya pauni" na inatarajiwa itasikilizwa mwaka wa 2024.

Mendy alijiunga na klabu ya Ligue 1 ya Lorient mwanzoni mwa msimu huu na hadi sasa ameshacheza mechi tatu kama mchezaji wa ziada

Alijiunga na City kutoka Monaco kwa mkataba wa £52m mwaka 2017 na kushinda mataji ya Premier League 2018, 2019 na 2021.

Mechi yake ya mwisho kwa klabu hiyo ilikwa kwenye Ligi Kuu mnamo 15 Agosti 2021.

Mendy alikaa rumande kwa miezi mitano kabla ya kuachiliwa kwa dhamana Januari 2022, na kisha kwenda kusikizwa kwa mara ya kwanza mnamo Agosti 2022.

Mnamo Januari aliondolewa mashtaka sita ya ubakaji na shtaka moja la unyanyasaji wa kijinsia.

Kisha aliondolewa kosa la kumbaka mwanamke na kujaribu kumbaka mwingine Julai katika kesi iliyosikilizwa upya.

Chanzo: Bbc