Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benin yawasili Dar, tayari kupambana na Stars

Tanzanie Benin Kikosi cha Benin

Wed, 6 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Taifa ya Benin, imewasili usiku wa Oktoba 5 katika Uwanja wa Julius Nyerere International Airport Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Afisa Habari wa TFF, Clifford Mario Ndimbo, amethibitisha kuwasili kwa kikosi hicho.

"Ni kweli timu ya Benin imeshawasili ikiwa na msafara wa watu 70, na wanatarajia kufanya mazoezi siku ya leo katika uwanja wa mkapa majira ya sa kumi jioni" amesema Ndimbo

Benin itakabiliana na Tanzania Oktoba 7, katika Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za kombe la dunia Qatar 2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live