Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benfica, Ajax ngoma bado mbichi

Ajaxx Benfica, Ajax ngoma bado mbichi

Thu, 24 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benfica imetoshana nguvu na Ajax kufuatia matokeo ya sare ya goli 2-2 katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora uliochezwa nchini Ureno.

Ajax walitangulia kupata goli la mapema kunako dakika ya 18 kupitia kwa Dusan Tadic akimalizia pasi ya Noussair kabla ya bao la kujifunga ambapo mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast Sebastian Haller alijitupia akiwa kwenye harakati za kuokoa na kufanya matokeo kuwa 1-1.

Muda mfupi kwenye dakika ya 29, Haller aliingia kambani mara hii alikuwa amefunga kwa mpinzani wake kabla ya goli hilo kusawazishwa tena dakika za jioni kupitia kwa Roman Yaremchuk dakika ya 72.

Mchezo wa marudiano utakaopigwa mwezi Machi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live